UWE HALISI KATIKA MAISHA
Uwe halisi maisha yako . Kanuni hii itakupa maisha halisi: fikra+ maneno+ matendo. Je unafikiria nini?, je unanena maneno( unasema) gani? na je unatenda nini Kila siku? Mtu hufikiria kwanza halafu hunena maneno na kisha matendo ya kile aidha alichofikiria au alichonena. Ili kuwa halisi katika maisha yako ni lazima kanuni hii uizingatie. Maisha halisi ni yale yanayotokana na muunganiko wa fikra ,maneno na matendo. Maisha yako halisi ni yale ambayo sio ya kuiga, sio maisha kigeu kigeu. Ni maisha yenye msimamo yanayojengwa na dhamiri ya ndani na kudhihirishwa kwa maneno na matendo. Hebu kanuni hii inavyofanya kazi. Fikra: Mwanadamu amejaliwa uwezo wa kufikiri mambo mbali mbali bila ukomo. Fikra zinatokana na utashi na yako, ndiyo kusema huwezi kufikiria kitu ambacho kipo nje ya ngazi fulani ya utambuzi wako. Mtu huwa na fikra za namna mbili yaani fikra chanya na fikra hasi. sahihi ili uweze kuneno kwa usahihi. Vinginevyo utakuwa wanachokiita lugha ya siasa yaani kuwa m...