UWE HALISI KATIKA MAISHA

Uwe halisi maisha yako.
Kanuni hii itakupa maisha halisi: fikra+ maneno+ matendo.
Je unafikiria nini?, je unanena maneno( unasema) gani? na je unatenda nini Kila siku? Mtu hufikiria kwanza halafu hunena maneno na kisha matendo ya kile aidha alichofikiria au alichonena. Ili kuwa halisi katika maisha yako ni lazima kanuni hii uizingatie. Maisha halisi ni yale yanayotokana na muunganiko wa fikra ,maneno na matendo. Maisha yako halisi ni yale ambayo sio ya kuiga, sio maisha kigeu kigeu. Ni maisha yenye msimamo yanayojengwa na dhamiri ya ndani na kudhihirishwa kwa maneno na matendo. Hebu kanuni hii inavyofanya kazi.
Fikra: Mwanadamu amejaliwa uwezo wa kufikiri mambo mbali mbali bila ukomo. Fikra zinatokana na utashi na  yako, ndiyo kusema huwezi kufikiria kitu ambacho kipo nje ya ngazi fulani ya utambuzi wako. Mtu huwa na fikra za namna mbili yaani fikra chanya na fikra hasi. sahihi ili uweze kuneno kwa usahihi. Vinginevyo utakuwa  wanachokiita lugha ya siasa yaani kuwa mwepesi wa kusema bila fikra sahihi au dhamiri safi juu ya uneni husika. Hili ni jambo la kwanza katika kukufanya uwe na maisha halisi. Kumbuka jambo unalohitaji kushindana nalo ni kushindana na fikra duni, fikra hasi katika maisha yako ili uwe halisi.
Maneno: Hili ni jambo la pili kutenda kwa msingi kuwa maneno hutanguliwa na fikra. Watu wengi tuna hulka ya kuwa waongeaji sana bila . Natambua kuwa mtu akiwa mwongeaji ni rahisi kukosea kupitia kauli zake maana hawezi kuuzuia ulimi wake. Ama kuhusiana na maneno hakuna inayoongoza unenaji wa maneno ila kuna mara zote tunapokuwa katika mazungumzo ili kuwa halisi katika maneno yetu:
Baadhi ya mambo ya kuepuka katika maneno:
  • Epuka kukaripia.
  • Epuka maneno ya kushambulia.
  • Epuka sifa katika maneno yako ikiwa sio lazima kutoa sifa.
  • Epuka maneno machafu.
Kuhusu ukweli: Sema kile unachoamini kuwa ndio kweli, usisema blaa blaa, usiseme jambo ikiwa unajua ni uongo. Ukweli katika maneno yako ni msingi katika maneno yanayotoka katika ndani ya moyo.
Kuhusu kiasi. Mara zote unene kile tu kinachohitajika wala usizungumze zaidi ya kile ulichotakiwa uzungumze. Huwezi kuwa halisi katika maneno yako ikiwa hautauzuia ulimi wako unene maneno kiasi gani.
Kwa ujumla watu watu wanakujua wewe ni nani kupitia ni unasema. Kwa maneno yako watakuhukumu na kukuingiza katika orodha ya watu waliopo kwenye kitabu cha akili zao ( a mental dictionary).
Matendo: Ama kuhusua jambo hili la tatu, katika kukamilisha kanuni ya kuwa halisi, matendo yetu hututambulisha sisi ni nani. Ukifikiri sahihi na kutenda kwa usahihi utajenga heshima kwa watu. Matendo yako yastahili wema wote mbele ya watu wote: watoto, wakubwa, wake kwa waume, vijana kwa wazee, watu wa dini na wasio wa dini. Hii itakupa uhalisia wa maisha yako ya kila siku: kutenda yale unayonena na yale unayofikiri kwa usahihi.
Makala hii imeandaliwa na ndugu Paul Ng'hera, mwandishi wa vitabu, mjasiriamali na Mwalimu. Endelea kutembelea mtandao wetu ili tupate kujifunza zaidi.
                           hazinamaarifa.blogspot.com
       Au wasiliana naye kwa email hii ili uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye e-mail yako.
                           paulsonnghera@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

Mambo matano( 5) unayohitaji ili kubadili maisha yako