Mambo matano( 5) unayohitaji ili kubadili maisha yako

Maisha ya kila mtu ni matokeo ya akili na utashi wa kila mtu katika maisha yake. Kwa maneno mengine maisha yetu ni zao la akili yetu na utashi wetu. Kwanini nimesema hivyo, naamini kila mtu ana mawimbi ya akili ambayo hutengeneza program fulani ambazo hushughulika na maisha ya kila siku. Hivyo kama mtu akijaza program hasi kwenye akili yake atatoa kitu hasi, vivyo hivyo mtu akijaza program chanya atatoa kitu chanya, kwa wataalamu wa kiingereza wanatumia istilahi ya 'GIGO' yaani Good in, Good out. Bila kupoteza muda napenda kuzungumzia mambo matano unayohitaji ili kubadili maisha yako.
 
Mambo matano (5) unatohitaji ili ubadili maisha yako.
  1.  Kuwa na Imani ( believe )
    Hakika katika maisha kuna changamoto nyingi; kukatishwa tamaa, kuibiwa, kudharauliwa, kukataliwa n.k. katika haya yote amini kuwa kuna muda,namna na jinsi ya kuondokana nayo. Ni lazima uwe na imani na kile unachofanya, uwe mnyoofu na kuyapokea yote huku ukiwa na imani kuwa ipo siku ndoto na malengo yako utayafikia Imani ina nguvu sana katika masomo yako,katika biashara yako, katika ndoa yako, katika utumishi wako, katika uongozi wako kwani kwa kuamini tu binafsi naamini unapata asilimia fulani ya kile unachotaka unapokea.

    Tamko: Imani inaumba na kujenga kitu halisi katika ulimwengu halisi kutoka fikra au mawazo ya mtu.
     
  2. Kujitoa ( commit )
    Nafikiri ili nieleweke vizuri hapa, niseme kujitoa ni kusema kuwa mimi nahusika na jambo au shughuli husika wala si mwingine yeyote. Kujitoa ni kuchukua jukumu moja kwa moja bila kudhania kuwa kuna mtu atakusaidia. Ili kutengeneza maisha yako chukua jukumu kusimamia maisha yako yasiharibike au kuharibiwa na yoyote. Hakuna mtu aliyejitoa kikamilifu akashindwa kupata kile anachotafuta. Shida ya watu wengi huwa tunafanya mambo bila dhati ya moyo yaani ilimradi yaende.Ikiwa kweli una kiu kubwa ya kutaka uzee wako uonekana wa maana, basi unalazimika kujituma sana kwenye kila jambo unalolifanya. Ikiwa hutajituma na kuweka misingi imara wakati ukiwa kijana, sahau kuwa na mafanikio uzeeni na zaidi utalalamika na kujutia uzee wako wote.
     
  3. Kuthubutu (dare )
    Kuthubutu ni kuwa na moyo au kumua kufanya kitu hususani chenye changamoto. Hii ni nguzo muhimu sana. Kila kitu tunakifanya kwasababu tunathubutu kufanya kwa maana ikiwa hutathubutu kujaribu, hutathubutu kujitoa, ikiwa hutathubutu kupata hasara huwezi kuanzisha bishara,ikiwa hutathubutu kulima huwezi kulima,ikiwa hutathubutu kuondoka katika umasikini wa fikra huwezi kusoma kitabu n.k. Mimi nimethubutu kuandika makala hii nimeweza nawe thubutu kutengeneza maisha yako utaweza. Reginald Mengi tajiri na mmiliki wa makampuni makubwa Tanzania alishawahi kutweet (mtandao wa twitter)"Young entrepreneur,remember, there is always elements of luck in success,but succeed you must first dare" .
    Tamko: Unaweza kutengeneza maisha yako ikiwa utathubutu kuyatengeneza.
     
  4. Matumaini ( hope )
    Kwa maana tunapokuwa na tumaini fulani katika maisha yetu tunatafuta na kuamini kulipata tunalotumaini. Magumu na kushindwa kwetu kwa baadhi ya mambo si kitu sana ikiwa tunatumaini la kufanikiwa. Tunatengeneza maisha yetu kwa kutumaini dhidi ya kukata tamaa, uoga, wasi wasi na kuendelea kwenda mbele hata kama kuna magumu
     
  5. Kutengeneza fursa ( opportunities )
    Msingi mkuu wa kutafuta fursa ni kuwa na wazo ambalo unaweza kulibadili kuwa kitendo hatimaye wazo hilo kuwa bidhaa. Naungana mkono na Bwana Kasenene ambaye ni mwaasisi wa falsafa ya elimu ya SAJATU hapa Tanzania ,anaeleza kuwa .....mwanadamu ana mtaji mkamilifu ambao ni muunganiko wa vitu vitano ,muunganiko huo ni: WAZO CHANYA, VITENDO CHANYA, BIDHAA CHANYA, WATU CHANYA na PESA CHANYA  ambavyo vinatokana na kutekeleza wazo chanya.
 Mpendwa msomaji wa makala hii nikushukuru sana kwa kuwa kusoma makala hii. Jukumu langu nikuona unafanya vizuri katika kuboresha maisha yako. Jitume, amini na katende mema katika maisha yako. Ahsante.
Kama unapenda kuwa unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye e-mail yako. Tuma e-mail yako kwenda  paulsonnghera@gmail.com
                             Au

Comments

Popular posts from this blog

UWE HALISI KATIKA MAISHA